Thursday, 13 November 2014

NALIA


Tangu jadi umekuwa nami
Lakini tangu nijitie 'Ulami'
Sahauni nikakutupilia
Kwa pupa nikaubugia
Ukoloni wa mawazo hata wa lugha
Nikakuacha ukiwa kijilugha.
Nakurudia ewe lugha yamgu
Maana wewe ndo mwandani wangu
'Sinilaumu ingawa ni mtundu
Nitalishona kila shimo na tundu
Kwako mie mtumwa
Nitafanya yote bila kuumwa
Nipe nafasi nitumike
Ewe Kiswahili utambulike
Taifa lote likuheshimu
Mwanaisimu niwafahamishe
Umuhimu wako usokuwa nafiki
Wakutambue u rafiki.
‪#‎Kiswahili_barani

No comments: